Kidato cha Tano hadi cha Sita
Kuanzishwa na Mahali Ilipo
Shule ya sekondari Jifunzeni ilianza kufundisha masomo ya kidato cha tano hadi cha sita mwaka 2016. Shule hii ipo umbali wa kilometa mbili (Km 2) kutoka kituo cha daladala Ituha.

Masomo yanayofundishwa Kidato cha Tano na Sita

Shule ya sekondari Jifunzeni inafundisha masomo yafuatayo kwa kidato cha tano hadi cha sita:

  • Somo la Jumla,
  • Historia,
  • Jiografia,
  • Kingereza,
  • Kiswahili,
  • Hisabati za kawaida,
  • Uchumi,
  • Hisabati za Juu,
  • Fizikia,
  • Kemia,
  • Elimu ya viumbe (Biolojia),
  • Uhasibu, na
  • Biashara.

 

Tahasusi Zilizopo
Tahasusi zote zinajumuisha somo la jumla au uraia kama somo la lazima. Kwa sasa shule inatoa elimu ya kidato cha tano hadi cha sita katika michepuo ifuatayo:
TAHASUZI   MASOMO
HGL   Historia, Jiografia, na Kingereza
HGK   Historia, Jiografia, na Kiswahili
HKL   Historia, Kiswahili, na Kingereza
HGE   Historia, Jiografia and Uchumi
EGM   Uchumi, Jiografia, na Hisabati za Juu
PCM   Fizikia, Kemia, na Hisabati za Juu
PGM   Fizikia, Jiografia, na Hisabati za Juu
PCB   Fizikia, Kemia, na Biolojia
CBG   Kemia, Biolojia, na Jiografia
ECA   Uchumi, Biashara na Uhasibu.
Ili kuomba nafasi ya kusoma kidato cha tano au cha sita kwa mwaka huu wa masomo bofya hapa kupakua fomu ya maombi.
 
 

Imetengenezwa na: Msuha Alexander
© 2025 Shule ya Sekondari Jifunzeni, Mbeya. Haki Zote Zimehifadhiwa