Waanzilishi
Waanzilishi wakuu wa shule ya Jifunzeni ni Mr. Emannue Kajange na Mr. John's A. Mwakabela pamoja na familia zao.
Emmanuel Kajange ni Mkristo aliyeokoka. Alizaliwa mwaka 1968 katika Kijiji cha Chikumbulu, Wilaya ya Ileje, Mkoa wa Mbeya, Tanzani.

Emmanuel Kajange ni mume wa Naumi Mwanjala. Wana jumla ya watoto watatu ambao ni Rehema Kajange, Bariki Kajange na Rachel Kajange.

Alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Shitunguru iliyoko Wilaya ya Mbozi kuanzia mwaka 1977 hadi 1984, badae alijiunga na shule ya sekondari Irambo iliyoko wilaya ya Mbeya ambako alisoma kidato cha kwanza hadi cha nne kuanzia mwaka 1986 hadi 1989.
Pia alisoma masomo ya kidato cha tano na sita mwaka 1990 hadi 1992 katika chuo cha Mkwawa kupitia mpango elimu maalumu ulioandaliwa na serikali ya Tzanzania, uliokuwa na lengo la kuwaandaa wanafunzi kusoma Tahasusi ya  CM ed (Kemia na Hesabu) pamoja na Ualimu. Alienda chuo cha ualimu Monduli, Arusha Mwaka, ili kukamilisha mpango elimu maalum mwaka 1992 hadi 1992.

E. Kajange alisoma shahada ya kwanza mwaka 2005 hadi 2008, katika Chuo Kikuu cha Mzumbe, kilichoko Morogoro Tanzania na kuhitimu katika  fani ya Uongozi na Utawala.

Aliajiriwa na Jumuiya ya wazazi katika nafasi ya ualimu, shule ya sekondari Mbalizi kuanzia mwaka 1993 hadi 2000. Pia alifanya kazi ya ualimu katika shule ya sekondari Swilla kuanzia mwaka 2001 hadi 2010. Kuanzia mwaka 2011 hadi sasa anafanya kazi katika shule ya Jifunzeni
Posts Held
1. Mratibu wa projeki, Mbalizi Secondari
2. Makamu Mkuu wa Shule, Swilla Sekondari, 2001 hadi 2005.
3. Mkurujenzi, Jifunzeni Sekondari, 2011 hadi sasa.
John’s A. Mwakabela ni Mkristo aliyeokoka. Alizalia katika kijiji cha Igogwe, wilaya ya Rungwe mkoa wa Mbeya, Tanzania.

Johns Mwakabela ni mume wa Tusibwene B. Mwalwisi. Wana watoto wane (4) ambao ni Meshack  Mwakabela, Gladness Mwakabela, Bupe Mwakabela na Jestina Mwakabela

Alisoma elimu ya msingi katika shule ya msingi Lukata mwka 1974 hadi 1980,  badae alijiunga shule ya sekondari Lutengano ambako alisoma kidato cha kwanza hadi cha nne kuanzia mwaka 1984 hadi 1987.
Alipata mafunzo ya uwalimu Daraja la III A katika Chuo cha Uwalimu Tukuyu mwaka 1988 hadi 1990. Pia alismoe stashahada ya uwalimi katika Chuo cha uwalimu Malangu

John’s Mwakabela alisoma katika Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji, Mbeya na kuhitmu shahada ya kwanza katika fani ya sanaa mwaka 2010.

Mwakabela alikuwa Mwalimu Mkuu msaidizi katika shule ya msingi Nsalala kuanzia mwaka 1998 hadi 2001. Pia alikuwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Idugumbi kuanzia mwaka 2001 hadi 2003. Aliajiriwa kama mwalimu wa Sekondari na Mkuu wa shule Iwiji kuanzia mwaka 2006 hadi 2007.

Kwa sasa Mwakabela ameajiriwa na halmashauri ya wilaya, Mbeya na anafanya kazi ya Afisa Elimu Kata katika kata ya Utengule B.

 

 

Imetengenezwa na: Msuha Alexander
© 2023 Shule ya Sekondari Jifunzeni, Mbeya. Haki Zote Zimehifadhiwa