Obtain Jifunzeni Application Forms 
i.
Awe amehitimu kidato cha nne ndani ya miaka mitatu tangu ya siku ya kuomba au kudahiliwa na shule
ii.
Awe na ufaulu wa alama "C" angalau katika masomo alizozipata katika wa mwaka mmoja wa kidato cha nne au miaka miwili tofauti.
iii.
Akubaliane na sheria na taratibu za shule.

Wanafunzi wanaweza kuomba kujiunga na shule kwa kujaza fomu zinazopatikana shuleni Jifunzeni, kwa mawakala au/na kupitia  tovuti ya shule.

Wakati wa kuomba nafasi mwanafunzi atatakiwa:
i.
Kupakua fomu ya maombi ya kujiunga kidato cha kwanza au cha tano kupitia "pakua/vipakuaji" au kupitia www.jifunzenischools.ac.tz/matukio.html.
ii.
Kufanya malipo ya fomu, TZS 10,000 kupitia wakala au tawi la Benki lililo karibu yako. Jina la Akaunti ni: Jifunzeni Secondary School, Namba za Akaunti ni; NMB: 62506600004, CBA: 105278100011, and CRDB: 0150422064900. Jina la mtu anayefanya malipo liwe jina la Mwombaji (Mwanafunzi).
iii.
Ukishafanya malipo tuma ujumbe mfupi au kwenda namba 0754638039,  ukielezeza Jina la Mwombaji, tarehe ya malipo, jina la benki na tahasusi uliyochagua (kidato cha tano). Pia unaweza kupiga picha au kuskani karatasi ya kuweka pesa benki na kuituma kwa njia ya what's app kwenye namba hiyo hiyo.
iv.
Kwa wanafunzi wa kidato cha tano wanatakiwa kurudisha shuleni fomu za maombi zilizokamilika kupitia anuani ya Posta ambayo ni Shule ya Sekondari Jifunzeni, S.L.P 6209, Mbeya au kwa barua pepe (baada ya kuskani) jssp2008@yahoo.com
v.
Tunza nakala ya fomu ya maombi kwa ajili ya matumizi ya badae.
Jinsi ya Kuomba Nafasi za Masomo
Mwanafunzi anayehitaji kujiunga kidato cha tano katika shule ya sekondari Jifunzeni anatakiwa awe na sifa zifuatazo:
Shule ya Sekondari Jifunzeni inapokea maombi ya kujiunga na kidato cha tano kuanzia mwezi machi hadi mei kila mwaka. Muda wa kuanza na mwisho wa kupokea maombi utatangazwa katika "Mwaliko wa Kujiunga Kidato cha Tano". kila mwaka.

Udahili wa Kidato cha Tano
i.
Awe amehitimu darasa la saba ndani ya miaka mitatu (3) kabla ya siku ya kutuma maombi.
ii.
Afaulu mtihani wa udahili unaotolewa na shule na kiwango cha ufaulu wa mtihani huo kitapangwa na shule.
iii.
Awe na umri usiopungua miaka kumi na moja (11).
iv.
Akubaliane na sheria na taratibu za shule.
Wanafunzi wanaotajia kujiunga kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Jifunzeni wanakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
Shule ya sekondari Jifunzeni inapokea maombi ya kujiunga na kidato cha kwanza mwezi Septemba hadi Novemba kila mwaka. Mara nyingi tutatoa tangazo la kujiunga na kidato cha kwanza kupitia "Mwaliko wa kujiunga Kidato cha Kwanza".
Udahili wa Kidato cha Kwanza
Udahili wa Wanafunzi
Sifa za Kujiunga Kidato cha Kwanza
Sifa za Kujiunga Kidato cha Tano
 

Imetengenezwa na: Msuha Alexander
© 2022 Shule ya Sekondari Jifunzeni, Mbeya. Haki Zote Zimehifadhiwa