Kuhusu Shule ya Sekondari Jifunzeni
Wazo la kuanzisha shule ya sekondari Jifunzeni lilianzia mwaka 2008 na Ndugu Emmanuel Kajange na Ndugu John's Mwakabela. Hii ilitokana na maelengo ya JSSP ya kukuza na kupanua huduma za kiroho na kimwili zinazojumuisha kulinda mazingira, kutoa elimu, afya na maji kwa jamii.

Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya kijamii na kiroho shirika liliamua kuanza kutoa elimu ya sekondari na kujumuisha ndani yake utunzaji wa mazingira na huduma za afya.

Kuanzishwa kwa Shule ya Jifunzeni
Shule ya Jifunzeni ni miongoni mwa shule zinazotoa elimu bora, malezi na tabia njema kwa wanafunzi katika Mkoa wa Mbeya na Tanzania. Shule ya sekondari Jifunzeni, Kidato cha kwanza hadi cha nne ilianzishwa mwaka 2011, na kidato cha tano hadi cha sita ilianzishwa mwaka 2016.

Shule hii imesajiliwa chini ya wizara ya elimu, sayansi teknolojia na mafunzo ya ufundi kwa namba ya usajili S4395 na kupewa namba ya kituo cha mtihani S4628. Shule hii ilianza na wanafunzi themanini na nne (84) waliojaliwa katika kidato cha kwanza na wanafunzi aromani na nne (44) wlihamia kidato cha pili kutoka katika shule zingine mwaka 2011

Shule inaendelea kutoka elimu ya sekondari kwa kidato cha kwanza hadi cha nne na kidato cha tano hadi cha sita.
 
 

Imetengenezwa na: Msuha Alexander
© 2022 Shule ya Sekondari Jifunzeni, Mbeya. Haki Zote Zimehifadhiwa